Psalms 2

Mfalme Aliyechaguliwa Na Mungu


1 aKwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya,
na kabila za watu kula njama bure?

2 b cWafalme wa dunia wanajipanga
na watawala wanajikusanya pamoja
dhidi ya Bwana
na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.

3 dWanasema, “Tuvunje minyororo yao
na kuvitupilia mbali vifungo vyao.”


4 eYeye atawalaye mbinguni hucheka,
Bwana huwadharau.

5 fKisha huwakemea katika hasira yake
na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,

6 g“Nimemtawaza Mfalme wangu
juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”

Ushindi Wa Mfalme


7 hNitatangaza amri ya Bwana:
Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu,
leo mimi nimekuzaa.

8 iNiombe, nami nitayafanya mataifa
kuwa urithi wako,
miisho ya dunia kuwa milki yako.

9 jUtawatawala kwa fimbo ya chuma
na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.”


10 kKwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima;
mwonyeke, enyi watawala wa dunia.

11 lMtumikieni Bwana kwa hofu
na mshangilie kwa kutetemeka.

12 mMbusu Mwana, asije akakasirika
nawe ukaangamizwa katika njia yako,
kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula.
Heri wote wanaomkimbilia.
Copyright information for SwhKC